Home Habari Kuu Rais Ruto afungua Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi

Rais Ruto afungua Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi

Rais William Ruto, Mapema Jumatatu amefungua kongamnao la kwanza la Afrika kuhusu mabadiliko ya tabia nchi katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa KICC jijini Nairobi

0
Rais William Ruto akihutubia Kongamano la Kwanza la Tabia Nchi katika ukumbi wa KICC

Rais William Ruto mapema leo Jumatatu alifungua Kongamano la kwanza la Afrika kuhusu Tabia Nchi katika ukumbi wa jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta, KICC jijini Nairobi.

Ruto aliwarai viongozi wa Afrika kuwekeza zaidi katika mitambo na mashine zinazotumia kawi safi na zisizochafua mazingira na pia kufanya kilimo bora kinachochangia pakubwa utunzaji mazingira.

Wajumbe wanaohudhuria kongamanio la mabadiliko ya tabia nchi

“Mazungumzo ya Tabia Nchi yalianza mwaka 1992 mjini Rio De Janeiro brazil, ni miaka 31 baadaye ambapo kongamano hilo linaandaliwa Afrika kwa mara ya kwanza,” alisema Ruto.

“Tunao uwezo mkubwa wa kutumia kawi safi na malighafi asilia ambazo zinaweza kutumika vyema bila kuchafua mazingira lakini pia ni lazima tushirikiane kuondoa au kupunguza matumizi ya mashine na mitambo inayotoa gesi ya kabonidioksidi.”

Simon Stiell – Katibu mkuu, UNFCCC

Akihutuba kongamano hilo, Waziri wa Mazingira Soipan Tuya alitilia mkazo kuwa  mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika sekta kuu za kiuchumi, kama vile kilimo, ufugaji wa samaki,utalii, nishati,misutu na nyinginezo yanapaswa kutumika kupunguza kukabiliana madeni mengi yanayolikumba bara hili.

Soipan Tuya-Waziri wa Mazingira

Kongamano hilo linafungamana na wiki ya Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi  ambayo inaadhimishwa kati ya Septemba 4 na 8 mwaka huu.

Website | + posts