Rais William Ruto mapema leo Jumatatu amefungua kikao cha tatu cha Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, UNEP jijini Nairobi.
Akihutubia kikao hicho, Ruto ameyataka mataifa kushirikiana kumaliza matumizi ya plastiki, ambayo yamechangia pakubwa kwa uchafuzi wa mazingira.
Ruto alikariri haja ya mataifa yote kupunguza matumizi ya plastiki ambayo ni njia mwafaka ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kuna haja ya kutafuta njia zingine mbadala zisizotumia plastiki, plasitiki mbadala na bidhaa za plastiki ambazo hazina athari hasi kwa mazingira, afya na jamii.
“Nawaalika wawekezaji kuja na kuwekeza Afrika kwa sababu bara hili lina maliasili inayoweza kutumiwa kwa mibadala rafiki kwa mazingira,” aliongeza Rais Ruto.