Home Habari Kuu Rais Ruto afanya ziara ya kushtukiza JKIA

Rais Ruto afanya ziara ya kushtukiza JKIA

0

Rais William Ruto jana Jumatatu alifanya ziara ya kushtukiza katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA. 

Ruto alifika uwanjani hapo wakati akimuaga Rais Joko Widodo wa Indonesia aliyeondoka nchini baada ya kuhitimisha ziara yake ya kitaifa.

“Nilitembelea Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta kutathmini vifaa vyake, utendakazi na huduma zinazotolewa kwa wateja baada ya kumuaga Rais wa Indonesia Joko Widodo aliyefanya ziara ya kitaifa humu nchini,” alisema Rais Ruto baada ya kufanya ziara hiyo ya kushtukiza.

“Uwanja wa ndege unaotoa huduma bora, wa kisasa, wenye starehe, rafiki na unaoangazia maslahi ya wateja ni mali ya umma ambayo inatia moyo utendakazi wa mashirika ya ndege, wageni kurejea, wawekezaji kusalia nchini na wafanyabiashara kutengeneza pesa.”

Serikali imeahidi kupanua uwanja wa JKIA katika hatua ambayo itaongeza uwezo wake wa kuwahudumia wateja.

Upanuaji huo utahusisha ujenzi wa kituo kingine cha kisasa cha kuwahudumia wateja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here