Home Habari Kuu Rais Ruto afanya mabadiliko katika vikosi vya ulinzi KDF

Rais Ruto afanya mabadiliko katika vikosi vya ulinzi KDF

Rais Ruto amempandisha cheo na kumteua meja jenerali David Kimaiyo Tarus kuwa luteni jenerali na sasa atakuwa kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Kenya.

0

Rais William Ruto ametangaza kupandishwa vyeo pamoja na uteuzi mpya katika vikosi vya ulinzi vya Kenya-KDF.

Kwenye taarifa, kiongozi wa taifa ambaye pia ni mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Kenya amempandisha madaraka meja jenerali Charles Muriu Kahariri kuwa Luteni jenerali na kumteua kuwa naibu mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Kenya- Luteni jenerali Kahariri anachukua mahali pa Luteni jenerali Jonah Mwangi ambaye muda wake wa kuhudumu umekamilika baada yake kuhudumu jeshini kwa miaka-42.

Rais Ruto pia amempandisha cheo na kumteua meja jenerali David Kimaiyo Tarus kuwa luteni jenerali na sasa atakuwa kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Kenya.

Luteni jenerali Kimaiyo anachukua mahali pa Luteni jenerali Peter Mbogo Njiru ambaye muda wake wa kuhudumu umekamilika baada ya kuhudumu jeshini kwa 39.

Katika mabadiliko mengine, meja jenerali Jimson Longiro amepandishwa cheo kuwa luteni jenerali na kuteuliwa kuwa naibu chansela wa chuo kikuu cha kitaifa cha mafunzo kwa wanajeshi baada yake kuhudumu kama kamanda wa jeshi la wanamaji.

Brigadia Thomas Njoroge Ng’ang’a amepandishwa cheo kuwa meja jenerali na kuteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la wanamaji.

Wengine waliopandishwa vyeo ni meja jenerali Juma Shee Mwanyikai, meja jenerali Mohammed Nur Hassan, Brigadia Luke Kipkemoi Kutto, meja jenerali Aphaxard Muthuri Kiugu, meja jenerali John Mison Nkoimo, Brigadia Peter Shikuku Chelimo na  Brigadia Yahya Abdi.