Home Habari Kuu Rais Ruto aandaliwa dhifa na Biden ikuluni White House

Rais Ruto aandaliwa dhifa na Biden ikuluni White House

0

Rais William Ruto aliandaliwa dhifa ya chajio kwenye Ikulu ya White House Alhamisi usiku na mwenyeji wake Joe Biden.

Dhifa hiyo ilifuatia mazungumzo ya kina baina ya Marais hao wawili, kuhusu mikakati ya maendeleo na ushirikiano kati ya kenya na Marekani kwa miaka 60 iliyopita.

Ruto aliandamana na mkewe Rachael wakati Biden akiambatana na mkewe Jil  wakati wa dhifa hiyo  ya kufana.

Rais Biden anatarajiwa kumuaga rasmi Ruto Ijumaa baada ya ziara rasmi ya kiserikali ya siku nne nchini humo.