Home Habari Kuu Rais Ruto aagiza NYS kutoa ardhi kwa waathiriwa wa mafuriko

Rais Ruto aagiza NYS kutoa ardhi kwa waathiriwa wa mafuriko

0
Rais William Ruto.

Rais William Ruto ameagiza huduma ya kitaifa(NYS) kwa vijana kutoa ardhi ya makazi kwa waathiriwa wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kote nchini.

Akizungumza Alhamisi Ruto amesema wakazi walio katika maeneo hatari na yanayokabiliwa na mafuriko watahamia kwenye ardhi itakayotolewa na NYS.

Rais amesisitiza kuwa serikali itawashurutisha wakazi walio katika maeneo hatari ya mafuriko kuhama.

Ruto ameongeza kuwa wizara husika ya mipango maalum inakusanya vyakula na bidhaa nyingine zitakazogawiwa waathirika wa mafuriko.