Home Habari Kuu Rais na naibu wake wapongeza wanariadha wa Kenya kwa ushindi

Rais na naibu wake wapongeza wanariadha wa Kenya kwa ushindi

0

Rais William Ruto amempongeza wanariadha Benson Kipruto, Timothy Kiplagat na Vincent Kipkemoi Ngetich kwa kunyakua nafasi tatu za mwanzo katika mbio za Marathon za Tokyo nchini Japan, upande wa wanaume.

“Bidii na kujitolea kwenu kwa riadha vimesababisha mheshimike ulimwenguni na hilo linatufanya tujivune, pongezi.” aliandika Rais Ruto kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Rais alimtaja pia Rosemary Wanjiru ambaye aliridhika na nafasi ya pili kwenye mbio hizo za Tokyo kwa upande wa kina dada. Alisema hii ni hatua muhimu katika taaluma yake kama mwanariadha na ni sababu ya wakenya kujivuna.

Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa upande wake alisema ushindi wa wanariadha wa Kenya katika mbio hizo ni dhihirisho la ustadi wa Kenya katika riadha. Aliwapongeza wote kwa matokeo mazuri.

Benson Kipruto alitumia muda wa saa 2 dakika 2 na sekunde 16 kukamilisha mbio hizo akifuatiwa na Timothy Kiplagat na Vincent Kipkemoi Ngetich.

Wanjiru alizidiwa nguvu na Sutume Kebede wa Ethiopia aliyetumia muda wa saa 2 dakika 15 na sekunde 55 na kuibuka mshindi huku yeye akitumia muda wa saa 2 dakika 16 na sekunde 14.

Website | + posts