Home Habari Kuu Rais Museveni amteua mwanawe kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

Rais Museveni amteua mwanawe kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

0

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) ya nchi hiyo.

Uteuzi huo umezua mjadala ndani na nje ya Uganda huku wengi wakiuchukulia kuwa matayarisho ya kumrithisha Jenerali Muhoozi uongozi wa nchi hiyo.

Jenerali Muhoozi anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Biashara.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Muhoozi alihudumu kama Mshauri Mkuu wa Rais katika Masuala ya Operesheni Maalum.

Luteni Jenerali Samuel Okiding ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Majeshi.

Katika taarifa, Msemaji wa Ulinzi Brigedia Jenerali FM Kulayigye pia ametangaza kuteuliwa kwa Luteni Jenerali Peter Elwelu kuwa Mshauri Mwandamizi wa Rais.

Website | + posts