Home Habari Kuu Rais Mnangagwa wa Zimbabwe aapishwa kuhudumu muhula wa pili

Rais Mnangagwa wa Zimbabwe aapishwa kuhudumu muhula wa pili

0

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuhudumu muhula wa pili.

Hii ni baada ya Rais huyo mwenye umri wa miaka 80 kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo mwishoni mwa mwezi jana.

Rais Mnangagwa alikula kiapo cha utendakazi katika Uwanja wa Kitaifa wa Michezo mjini Harare leo Jumatatu mbele ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo Luke Malaba.

Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe ilimtangaza Mnangagwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kujizolea asilimia 52.6 ya kura zilizopigwa huku mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa akipata akipata asilimia 44 ya kura.

Chamisa amepinga vikali matokeo hayo akidai yalikumbwa na cheche kali za udanganyifu.

Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi alikuwa mjini Harare kumwakilisha Rais William Ruto wakati wa kuapishwa kwa Rais Mnangagwa.

Ruto amempongeza Rais Mnangagwa kwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili na pia kuwapongeza watu wa taifa la Zimbabwe kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani.

Mnangagwa aliingia madarakani wakati mtangulizi wake Robert Mugabe alipobanduliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Chama tawala cha ZANU-PF kimeongoza nchi hiyo kwa miaka 43 sasa.