Home Habari Kuu Rais Kagame: Kenya ilitekeleza wajibu mkubwa kuisaidia Rwanda

Rais Kagame: Kenya ilitekeleza wajibu mkubwa kuisaidia Rwanda

0

Rais wa Rwanda Paul Kagame, ameipongeza Kenya kwa wajibu wake mkubwa katika kujengwa upya kwa taifa la Rwanda baada ya mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa mwaka 1994.

Rais Kagame alisema Kenya iliwahifadhi wakimbizi wengi waliokuwa wakitoroka Rwanda wakati wa kipindi hicho kigumu.

Rais Kagame aliwaambia marais na viongozi wa serikali, mabalozi na wakuu wa jumbe mbalimbali jijini Kigali kuwa Kenya ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyosaidia kujengwa na kufufuliwa upya kwa taifa la sasa la Rwanda.

Alikuwa akiongea katika eneo la BK Arena jijini Kigali Rwanda wakati wa maadhimisho ya 30 ya kitaifa tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari  ya Rwanda yaliyosababisha vifo vya mamilioni ya watu mwaka wa 1994.

Kenya, pamoja na mataifa mengine, ilihifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Rwanda na kuwapatia makao,” alisema Rais huyo wa Rwanda.

Kenya iliwakilishwa na naibu wa rais Rigathi Gachagua ambaye alimwakilisha rais William Ruto.

Gachagua aliweka shada la maua katika eneo la ukumbusho la Kigali Genocide Memorial, kwa heshima ya waathiriwa wa mauaji hayo ya halaiki ya mwaka wa 1994.

Kituo hicho cha ukumbusho ndipo walipozikwa mamilioni ya watu waliouawa katika kipindi cha miezi mitatu cha mauaji hayo ya halaiki.

Siku ya jumapili iliadhimisha mwanzo wa maadhimisho ya siku mia moja ya kumbukumbu hizo.

Baadhi ya viongozi wa dunia waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton, Rais wa Sudan Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, Rais wa Samia Sulubu na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed miongoni mwa wengine.

Website | + posts