Home Kimataifa Rais Joko Widodo wa Indonesia azuru Kenya

Rais Joko Widodo wa Indonesia azuru Kenya

0
kra

Rais wa nchi ya Indonesia, Joko Widodo yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi. Alilakiwa katika Ikulu ya Nairobi na Rais William Ruto na naibu Rais Rigathi Gachagua kikamilifu na mizinga 21 kutoka kwa jeshi.

Dhamira ya ziara ya Widodo nchini Kenya ni kufanya mazungumzo na Rais Ruto kuhusu ushirikiano kati ya Indonesia na Kenya.

kra

Viongozi hao wawili watazindua mashine za kuuza mafuta ya kupikia ya bei nafuu au ukipenda “Mama Pima Edible Oil Dispensing Machines” jijini Nairobi ambazo zinaundwa na kusambazwa na kamouni ya serikali ya biashara “Kenya National Trading Corporation”.

Ujio wa mashine hizo unalenga kuhakikisha kwamba wateja wanapata mafuta ya bei nafuu na nafasi za ajira zinatengenezwa kwa makundi yaliyojisajili.

uzinduzi huo unafanyika katika afisi ya naibu kamishna wa Nairobi eneo la dagoretti.

Website | + posts