Home Habari Kuu Rais Cyril Ramaphosa asema lazima vita nchini Ukraine vikome

Rais Cyril Ramaphosa asema lazima vita nchini Ukraine vikome

0

Kiongozi wa Afrika Kusini alisema hayo wakati yeye na viongozi wengine sita kutoka Bara Afrika walikutana na Rais Vladmir Putin wa Urusi jijini St Petersburg Jumamosi Juni, 17.

Ijumaa, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliambia ujumbe huo wa Afrika kwamba hawezi kuanza mashauriano na Russia wakati bado wameteka ardhi ya Ukraine. Putin kwa upande wake alisema Ukraine ndiyo imekataa mazungumzo ya kumaliza vita.

Rais Ramaphosa alizitaka nchi hizo mbili pia kubadilishana wafungwa wote wa vita na watoto waliotolewa Ukraine na Russia warejeshwe. Putin hata hivyo alijitetea akisema kwamba Russia inalinda watoto hao. Ameshtakiwa katika mahakama ya ICC kwa kuondoa kwa lazima watoto wengi kutoka Ukraine na kuwapeleka Russia.

Viongozi wa Afrika Kusini, Misri, Senegal, Congo-Brazzaville, Comoros, Zambia na Uganda walisema wanataka vita kati ya Ukraine na Russia vikome kwa sababu vina athari mbaya kwa Bara Afrika.

Vita hivyo vimetatiza pakubwa uuzaji wa nafaka kutoka Ukraine na mbolea kutoka Russia jambo ambalo limesababisha uhaba wa chakula ulimwenguni.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here