Home Habari Kuu Rais Chakwera asitisha safari zote nje ya nchi

Rais Chakwera asitisha safari zote nje ya nchi

0
kra

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza kukomeshwa kwa safari zote za nje ya nchi hiyo kwake yeye kama Rais na kwa maafisa wote wa serikali nchini humo.

Kwenye hotuba kwa taifa kupitia runinga, kiongozi huyo alielezea kwamba marufuku hiyo itadumu hadi mwisho wa mwaka wa sasa wa matumizi ya pesa za serikali hiyo, Machi, 2024.

kra

Alisema kwamba amekatiza safari yake ya kwenda kuhudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi almaarufu COP28 mwisho wa mwezi huu huku marufuku hiyo ikianza kutekelezwa.

Chakwera aliamuru mawaziri wa nchi hiyo ambao wako nje kwa ziara warejee nyumbani mara moja.

Kuhusu safari za ndani ya nchi hiyo ya Malawi, Rais Chakwera aliweka vikwazo huku akipunguza kwa karibu nusu mgao wa fedha ambao unatengewa mawaziri na maafisa wakuu serikalini kununua mafuta.

Rais huyo aliagiza kupunguzwa kwa ushuru wa mapato kwa raia wa nchi hiyo kwenye bajeti ya mwaka 2024/2025 ili kuwalinda kutokana na gharama ya maisha inayozidi kuongezeka.