Home Kimataifa Rais Biden na Netanyahu wazungumza kwa njia ya simu

Rais Biden na Netanyahu wazungumza kwa njia ya simu

Ikulu ya White House ilisema Makamu wa Rais wa Merikani Kamala Harris pia alijiunga na mazungumzo hayo ya simu  ya dakika 30 siku ya Jumatano.

0
kra

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo ya simu yaliyotarajiwa na waziri mkuu wa Israel, ambayo yanaaminika kuwa mazungumzo yao ya kwanza baada ya wiki kadhaa. 

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Biden wanaaminika kujadili namna Israel ilivyojibu shambulilizi la makombora la Iran wiki iliyopita huku mzozo ukiendelea kutokota katika eneo la Mashariki ya Kati.

kra

Ikulu ya White House ilisema Makamu wa Rais wa Merikani Kamala Harris pia alijiunga na mazungumzo hayo ya simu  ya dakika 30 siku ya Jumatano.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba majadiliano juu ya shambulizi  la Iran yalifanywa.

Aliongeza kuwa mradi wa uwanja mkuu wa ndege wa Beirut utaendelea kuwa wazi huku Marekani ikiendelea kufanya safari za ndege za kuwachukua Wamarekani ambao bado wako nchini Lebanon.

Mapigano yanaendelea Mashariki ya kati, kati ya Hezbollah na Israel, huku watu wanne wakiuawa katika shambulizi la angani la Israel kwenye kijiji cha Lebanon karibu na mji wa kusini wa Sidon.

Israel ilisema imefanya zaidi ya mashambulizi 1,100 ya angani tangu uvamizi wake wa ardhini uanze kusini mwa Lebanon tarehe 30 Septemba.

Website | + posts