Home Habari Kuu Rais Biden kuzuru Israel Jumatano

Rais Biden kuzuru Israel Jumatano

Ziara ya Biden inawadia kwa mwaliko wa Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

0
Rais wa Marekani Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden atazuru Israel siku ya Jumatano, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kutoka Israel.

Tangazo kwamba Rais Biden atazuru Israel lilitolewa katika ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem, baada ya mkutano wa saa saba kati ya mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu Netanyahu siku ya Jumatatu.

Biden “atapokea taarifa za kina juu ya malengo na mkakati wa vita vya Israeli” wakati akiitembelea nchi hiyo, Blinken aliwaambia waandishi wa habari.

Pia “atasikia kutoka kwa Israeli jinsi itakavyoendesha operesheni zake kwa njia ambayo itapunguza majeruhi ya raia” na kuruhusu msaada kuwafikia raia wa Palestina huko Gaza.

Ziara ya Biden inawadia kwa mwaliko wa Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Website | + posts