Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alifanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri siku ya Jumatano huku akimtimua waziri wa Fedha.
Kwenye mabadiliko hayo Rais Addo alimtimua waziri wa Fedha Ken Ofori-Atta, kufuatia shinikizo la kutaka kutimuliwa kutokana na uongozi mbaya wakati uchumi wa taifa hilo ulikuwa umedorora.
Amin Adam ndiye atakuwa waziri moya wa Fedha akihamishwa kutoka wizara ya kawi.
Chini ya uongozi wa Ofori mfumko wa bei ulipanda hadi asilimia 50 kwa mara ya kwanza huku taifa hilo likikabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na kushuka kwa thamani ya sarafu.