Home Taifa Rais aahidi wakazi wa Kirinyaga miradi ya maendeleo

Rais aahidi wakazi wa Kirinyaga miradi ya maendeleo

0
kra

Rais William Ruto ameahidi wakazi wa kaunti ya Kirinyaga kwamba serikali yake itatekeleza miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo hilo siku za hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa ziara ya maendeleo katika kaunti hiyo, kiongozi wa nchi alitaja mradi wa kuunganisha familia zaidi ya elfu saba na umeme chini ya mpango wa “Last Mile Conectivity”.

kra

Kiongozi wa nchi alisema kwamba mpango huo ambao ulikuwa umekwama kwa muda lakini sasa utaendelezwa na awamu aliyotangaza ya Kirinyaga imetengewa shilingi milioni 500.

Wakati wa ziara hiyo Rais Ruto aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kiviwanda cha Sagana akiwa ameandamana na viongozi kadhaa wa kaunti ya Kirinyaga kama Gavana Anne Waiguru na mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Kulingana na Waiguru kituo hicho cha kiviwanda kitatoa jumla ya fursa elfu 150 za ajira, elfu 30 zikiwa za moja kwa moja huku elfu 120 zikiwa sio za moja kwa moja.

Tayari serikali ya kaunti ya Kirinyaga imetenga shilingi elfu 180kwa ajili ya mradi huo serikali kuu ikitarajiwa kutoa ufadhili uliosalia.

Miradi mingine aliyozindua kiongozi wa nchi katika kaunti ya Kirinyaga ni pamoja na ujenzi wa barabara za urefu wa kilomita 65 zinazounganisha sehemu mbali mbali za kaunti hiyo, taasisi ya kozi za kiufundi ya Kirinyaga Central na maabara ya Jitume katika taasisi hiyo.

Website | + posts