Home Habari Kuu Raila atoa wito wa kuchunguzwa kwa vifaa vya kiusalama

Raila atoa wito wa kuchunguzwa kwa vifaa vya kiusalama

Marehemu Jenerali Ogolla atazikwa kesho Jumapili nyumbani kwake katika kaunti ya Siaya.

0
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ametoa wito wa kuchunguzwa kwa vifaa vya kiusalama, hususan ndege za kijeshi katika juhudi za kupunguza maafa zaidi, kufuatia kifo cha mkuu wa vikosi vya ulinzi Jenerali Francis Ogolla.

Akizungumza wakati wa ibada iliyoandaliwa kwa heshima ya mkuu wa vikosi vya ulinzi hapa nchini marehemu Jenerali Francis Ogolla, Raila alidokeza kuwa katika kipindi cha kati ya miaka mitano na kumi, watu wengi wameangamia kutokana na ajali za helikopta.

“Wakati umewadia kuchunguza vifaa vya kiusalama vya nchi hii, haswa jeshi za kijeshi ambazo ziwmewaua watu wengi katika kipindi cha kati ya miaka tano na kumi iliyopita,” alisema kiongozi huyo wa chama cha ODM.

Aidha waziri huyo mkuu wa zamani, alitoa wito wa kufanywa kwa uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo, iliyosababisha kifo cha mkuu wa vikosi vya ulinzi Jenerali Francis Ogolla pamoja na maafisa wengine tisa wa KDF, kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Marehemu Jenerali Ogolla atazikwa kesho Jumapili nyumbani kwake katika kaunti ya Siaya.

Website | + posts