Home Kaunti Raila atoa msaada kwa waliofurushwa msitu wa Mau

Raila atoa msaada kwa waliofurushwa msitu wa Mau

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametoa msaada wa chakula,mabati na blanketi kwa wakimbizi wapatao 3,000 ambao walifurushwa kutoka msitu wa Maasai Mau eneo bunge la Narok Kaskazini.

Msaada huo uliwasilishwa kwa wahanga hao na Moitalel Ole Kenta, wa chama cha ODM ambaye aliwania ugavana wa kaunti ya Narok kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Katika kijiji cha Enesonkoyo, Kenta aligawa blanketi 610, Mabati 500, Unga wa mahindi pakiti 2,400, Sukari kilo 500 na Mafuta ya kupika pakiti 300.

Kenta alikana madai ya kuingilia uongozi wa eneo hilo akiweka wazi kuwa nia yake ni umoja kwa haki kwa familia zilizofurushwa na serikali kimakosa na kuwa haipaswi.

Huku akidai kwamba kuna mipango ya kufurusha wakazi wa eneo la Naisoya, Kenta alisema kwamba ni sharti uchunguzi utekelezwe ili kufahamu mipaka halisi.

Alionekana kutounga mkono ufurushaji huo akisema uliathiri watahiniwa wa mitihani ya kitaifa ya shule za msingi na sekondari.

Kenta alisisitiza kuwa jamii hiyo imesalia mstari wa mbele kulinda misitu akimkumbusha Rais atekeleze matakwa ya jamii kama alivyoahidi kabla ya ufurushaji.

Website | + posts
Stanley Mbugua
+ posts