Home Taifa Raila akutana na Balozi wa EU wakati akiwinda uenyekiti wa AUC

Raila akutana na Balozi wa EU wakati akiwinda uenyekiti wa AUC

0
kra

Kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga amekutana na Balozi wa Umoja wa Afrika, EU humu nchini Henriette Geiger wakati akiimarisha kampeni zake za kugombea uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC. 

Raila amekuwa akikutana na viongozi mbalimbali katika siku za hivi karibuni katika juhudi zinazoonekana kuwa za kuinua hadhi yake na kutafuta uungwaji mkono wa wadhifa huo.

kra

Katika mkutano wake na Geiger leo Alhamisi, wawili hao walizungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuufanyia marekebisho Umoja wa Afrika, AU.

“Nilikuwa na mazungumzo yenye tija na Balozi wa Umoja wa Ulaya, EU nchini Kenya Henriette Geiger juu ya marekebisho muhimu yanayopaswa kufanywa kwa AU, kuimarisha biashara baina ya mataifa ya bara la Afrika, hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuwekeza katika elimu na miundombinu,” alisema Raila baada ya mkutano baina yao.

“Tulikubaliana juu ya haja ya kuwa na Afrika yenye umoja na utangamano, iliyoiga mfano wa AU.”

Raila anatarajiwa kukabiliana na wagombeaji wengine ambao ni Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Madagascar Richard James Randriamandrato, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssou na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Mauritius Anil Kumarsingh Gayan katika azima yake ya kumrithi Moussa Faki kama mwenyekiti wa AUC.

Uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Faki umepangwa kufanyika mwezi Februari mwakani.

Website | + posts