Home Kimataifa Raila akashifu kuingiliwa kwa maandamano na wahuni

Raila akashifu kuingiliwa kwa maandamano na wahuni

0
kra

Kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga amelaani hatua ya wahuni kuingilia maandamano ya vijana almaarufu Gen Z na kusababisha madhara makubwa katika sehemu mbali mbali nchini.

Kupitia taarifa yake leo, Raila anasema kwamba maandamano yaliyoanzishwa na vijana hao kwa lengo la konyesha kutoridhika kwao na mapungufu ya serikali na kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka husina yaligeuzwa vurugu na wahuni jana.

kra

Huku akitoa pole kwa walioathirika na unyama uliotekelezwa na wahuni hao kwa njia moja au nyingine, Raila alisema hatua za majambazi hao za kupora na kuharibi mali ya raia ni sawa na usaliti mara mbili kwa vijana.

Kiongozi huyo alisifia vijana wa Gen Z akisema kwamba wameelimisha wengi humu nchini na nje kwamba maandamano yanaweza kuwa ya amani huku akiwataka wahuni kukomesha taiba mbaya.

“Kuna ripoti kwamba wanawake wasiokuwa na hatia walidhulumiwa na kubakwa katika sehemu mbali mbali nchini wakati wa maandamano ya jana.” alisema Raila kwenye taarifa yake akiongeza kwamba runinga kadhaa zilionyesha uporaji ulioendelea jana.

Alisema kwamba wamekuwa wakipaaza sauti kuhusu ukatili wa maafisa wa polisi dhidi ya waandamanaji na sasa wanapaaza sauti pia dhidi ya wahuni walioingilia maandamano.