Home Burudani Raia wa Uingereza na Amerika waonywa dhidi ya kuhudhuria Nyege Nyege

Raia wa Uingereza na Amerika waonywa dhidi ya kuhudhuria Nyege Nyege

0

Balozi za nchi za Marekani na Uingereza nchini Uganda zimeshauri raia wake nchini humo dhidi ya kuhudhuria tamasha ya Nyege Nyege.

Ushauri huo wa hofu ya mashambulizi ya kigaidi unaonya watu hao dhidi ya kusafiri hadi jijini Jinja ambapo tamasha hiyo itaandaliwa na hadi vivutio vingine vya utalii nchini Uganda kama mbuga za wanyama.

Tamasha ya Nyege Nyege itaandaliwa kwa siku nne jijini Jinja kuanzia kesho, Novemba, 9, 2023.

Katika onyo la Jumatatu, ubalozi wa Marekani jijini Kampala ulisema kwamba kutokana na hofu ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi, raia wa nchi hiyo wanashauriwa dhidi ya kuhudhuria mikusanyiko jijini Kampala na Jinja.

Hata hivyo msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga katika kikao na wanahabari hiyo hiyo Jumatatu alikana madai ya kuwepo kwa hofu ya mashambulizi ya kigaidi.

Website | + posts