Home Habari Kuu Raia wa Uholanzi ashtakiwa kwa kuwadhulumu watoto

Raia wa Uholanzi ashtakiwa kwa kuwadhulumu watoto

0

Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi, siku ya Ijumaa alifikishwa mahakamani kwa madai ya kumdhulumu kimapenzi mvulana wa umri wa miaka 16.

Jan In’t almaaru dad, auTacher Jan Mzungu, alifikishwa katika mahakama ya Milimani ya kushughulikia watoto, akikabiliwa na mashtaka tisa ya kuwadhulumu watoto kimapenzi na pia kuhusika na filamu za ngono za watoto

Jan anatuhumiwa alitekeleza makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya mwezi April na mwezi Juni mwaka uliopita katika kaunti ndogo ya Turbo, kaunti ya Uasin Gishu

Kulingana na kiongozi wa mashtaka , makosa hayo ni kinyume na sehemu ya 11(1)  ya sheria za makosa ya ngono  nambari tatu ya mwaka 2016.