Home Habari Kuu Raia wa Poland akamatwa na mihadarati katika uwanja wa ndege wa JKIA

Raia wa Poland akamatwa na mihadarati katika uwanja wa ndege wa JKIA

Mshukiwa huyo alitiwa nguvuni muda mfupi baada ya kuabiri ndege ya shirika la ndege la Misri iliyokuwa ikielekea Hungary.

0

Maafisa wa polisi wa kukabiliana na mihadarati, wamemkamata raia wa Poland anayeshukiwa kuwa mlanguzi wa dawa za kulevya.

Arkadiusz Stanislaw mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa na maafisa wa polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA akiwa na dawa za kulevya aina ya heroine za thamani ya shilingi milioni mbili.

Mshukiwa huyo alitiwa nguvuni muda mfupi baada ya kuabiri ndege ya shirika la ndege la Misri iliyokuwa ikielekea nchini Hungary.

Kwa sasa anazuiliwa katika korokoro za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mkurugenzi wa kitengo cha polisi wa kukabiliana na mihadarati Margaret Karanja, ameonya kuwa wale watakaonaswa wakihusika na biashara ya mihadarati watachukuliwa hatua kali za kisheria bila kuzingatia jukumu lao katika biashara hiyo.