Home Habari Kuu Raia wawili wa kigeni wakamatwa na pembe za ndovu

Raia wawili wa kigeni wakamatwa na pembe za ndovu

Pembe hizo za ndovu zilinaswa na maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS, ambao wanakabiliana na biashara haramu ya pembe za ndovu.

0

Raia wa Indonesia amekamatwa akiwa na kilo 38.4 ya pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni kumi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.

Mshukiwa huyo ambaye alikuwa ameabiri ndege ya shirika la Kenya Airways nambari 571, iliyokuwa ikielekea  Jakarta kutoka Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, alikamatwa wakati wa ukaguzi wa abiria katika uwanja huo.

Pembe hizo zilinaswa na maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori, KWS ambao wanakabiliana na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa na maafisa wa polisi huku akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mnamo Septemba 22, 2023, maafisa wa polisi na wale wa KWS waliwakamata washukiwa wawili waliokuwa na kilo 53 za pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni kumi katika kaunti ya Embu.

Website | + posts