Home Habari Kuu Raia wa DRC kuzuru Kenya bila viza kuanzia Septemba 1

Raia wa DRC kuzuru Kenya bila viza kuanzia Septemba 1

Kabla ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki raia wote wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo wamekuwa wakihitajika kulipia VISA ili kuingiz nchini Kenya.

0

Ni afueni kwa raia  wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC wanaopania kuzuru nchini baada ya serikali kuondoa masharti ya viza ili kuzuru nchini kuanzia Septemba mosi mwaka 2023.

Kulingana na serikali, agizo hilo linatokana na DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC mwezi Mei mwaka jana ambapo kwa kawaida, raia wa mataifa hayo hawahitaji viza ili kutembea miongoni nchi saba za jumuiya ya EAC.

Kabla ya kujiunga na jumuiya hiyo, raia wote wa kutoka DRC wamekuwa wakihitajika kulipia viza ili kuingia nchini Kenya.

Website | + posts