Home Habari Kuu Mfanyabiashara Rai aondoa kesi zote alizowasilisha mahakamani

Mfanyabiashara Rai aondoa kesi zote alizowasilisha mahakamani

Rai siku ya Alhamisi aliwasilisha arifa ya kuondoa kesi zote tatu ikiwemo ie iliyowasilishwa na kampuni yake moja ya West Sugar katika mahakama ya viwandani Milimani.

0

Mfanyabiashara bilionea Jaswant Rai amewasilisha arifa ya kuondoa kesi zote alizowasilisha kwenye mahakama kuu na ile ya rufaa baada ya Rais William Ruto kutaka kesi hizo ziondolewe. 

Rai leo Alhamisi aliwasilisha arifa ya kuondoa kesi zote tatu ikiwemo ile iliyowasilishwa na kampuni yake moja ya West Sugar katika mahakama ya kushughulikia mizozo ya kikazi ya Milimani.

Kesi ya mahakama ya rufaa ilikuwa dhidi ya Sarbjit Singh Rai, Rakesh Kumar na Stephen Kihimba wanaokabiliwa na kesi ya kupuuza mahakama walipoagizwa kujitenga na kusita kuendesha shughuli katika kampuni ya sukari ya Mumias.

Rais Ruto akiwa ziarani eneo la magharibi ya Kenya alitoa onyo kwa matapeli  aliyosema wanahujumu  juhudi za serikali za kufufua kampuni ya kusaga miwa ya Mumias kupitia kwa kesi zilizowasilishwa mahakamani.

Website | + posts