Home Kaunti Rahim Dawood aunga mkono Rais Ruto kuhusu kupambana na ufisadi

Rahim Dawood aunga mkono Rais Ruto kuhusu kupambana na ufisadi

Mbunge wa Imenti Kaskazini Rahim Dawood amesema kwamba anamuunga mkono Rais William Ruto katika masuala ya kupambana na ufisadi hasa katika idara ya mahakama na asasi nyingine za serikali.

Akizungumza huko Meru, Rahim alisema Rais alikuwa sahihi kwamba kuna visa vya ufisadi katika idara ya mahakama na asasi nyingine za serikali.

Anapendekeza kwamba Rais afanye mkutano na jaji mkuu Martha Koome ili suala hilo la ufisadi litatuliwe kwa njia ya amani.

Mbunge huyo ameitaka idara ya mahakama kutokuwa kinyume na miradi ya serikali kila mara kama inavyoshuhudiwa kwa sasa kwani hatua hiyo italemaza utekelezaji wa maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Jingine analotaka kutoka kwa idara hiyo ni kuharakishwa kwa kesi muhimu zinazogusa umma kama vile kesi dhidi ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na bima ya matibabu.

Website | + posts
Jeff Mwangi
+ posts