Home Kaunti Radi yasababisha kifo kaunti ya Narok

Radi yasababisha kifo kaunti ya Narok

Mwendazake Victor Bii mwenye umri wa miaka 34,  na rafikiye Weldon Mutai, walikuwa wakijikinga mvua wakati kisa hicho kilipotokea.

0

Mtu mmoja amefariki huku mwingine akijeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika soko la Triangle lililoko karibu na msitu wa Mau, kaunti ndogo ya Narok Kusini.

Mwendazake Victor Bii mwenye umri wa miaka 34,  na rafikiye Weldon Mutai, walikuwa wakijikinga mvua wakati kisa hicho kilipotokea.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Longisa katika kaunti ya Bomet, huku aliyejeruhuwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo.

Akithibitisha kisa hicho, Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Narok Kusini Felix Kisalu, amewataka wananchi kuwa waangalifu hasa wakati huu wa msimu wa mvua ili kuepukana na maafa na kupoteza mali.

“Watu wanapaswa kuhamia maeneo salama kabla ya mvua ya El-Nino kuanza, eneo hili hukumbwa sana na radi, mafuriko na maporomoko ya ardhi,” alisema Kisalu.

Tukio hilo lilitokea baada ya serikali ya kaunti hiyo kuzindua kituo cha kusgughulikia dharura, ikijiandaa kwa mvua za El Nino.

Website | + posts