Home Habari Kuu Putin avunja ukimya kuhusu ajali ya ndege

Putin avunja ukimya kuhusu ajali ya ndege

0
kra

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana.

Ametuma salamu za rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha, na anaelezea mwanzilishi wa Wagner Group Yevgeny Prigozhin kama mfanyabiashara mwenye talanta.

kra

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni Putin, anasema wachunguzi wataangalia kilichotokea, lakini hilo litachukua muda.

Anasema aliambiwa kuhusu ajali ya ndege iliyotokea Jumatano asubuhi.

Prigozhin alikuwa amerejea tu kutoka safari ya Afrika, asema Putin

Putin pia anasema kwamba “ninavyofahamu”, Prigozhin “ni jana tu [Jumatano] alirejea kutoka Afrika.Alikutana na watu fulani rasmi huko”.

Katika siku za hivi karibuni mkuu wa Wagner anaaminika kuwepo Afrika Magharibi, ambako wachambuzi wa nchi za Magharibi wanahofia kuwa kundi hilo lilikuwa likitaka kupanua wigo wake hadi katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Niger, ambako mapinduzi yametokea hivi karibuni.

Wagner ni nguzo muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Urusi, huku vikosi vyake vikisaidia kuunga mkono serikali za Syria, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya kwa kubadilishana na haki za uchimbaji madini.

BBC
+ posts