Home Michezo PSG yaamrishwa kumlipa Mbappe malimbikizi ya ujira wa dola milioni 61

PSG yaamrishwa kumlipa Mbappe malimbikizi ya ujira wa dola milioni 61

0
kra

Tume ya sheria katika Ligi Kuu ya Ufaransa imeamrisha klabu ya Paris Saint-Germain, PSG kumlipa aliyekuwa mshambulizi wake Kylian Mbappé malimbikizi wa ya ujira wa dola milioni 61.

Uamuzi huo uliafiikiwa jana Alhamisi baada ya mshambulizi huyo wa Real Madrid, kukataa abadan mazungumzo ya kutatua  mzozo huo mbele ya tume hiyo pamoja na mwajiri wake wa zamani.

kra

Kupitia kwa wawakilishi wake, Mbappe alisema alitaka alipwe malimbikizi ya mshahara wa miezi mitatu na thuluthi ya mwisho ya marupurupu yake.

Hata hivyo, PSG wameonyesha nia ya kutokuwa tayari kulipa malimbikizi hayo, wakiapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Klabu hiyo inasema malipo anayodai Mbappé, yalikuwa yale aliyokosa kucheza msimu wa mwaka 2023/204 kutokana na kutatizwa na majeraha.

Website | + posts