Home Habari Kuu Prof. kindiki atajwa waziri bora zaidi kwa utendakazi

Prof. kindiki atajwa waziri bora zaidi kwa utendakazi

Waziri wa kilimo Mithika Linturi, aliibuka wa pili, huku kampuni hiyo ikiashiria mageuzi katika sekta ya kilimo, kama vile dijitali ambayo yamechochea ukuaji katika kilimo.

0
Waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure Kindiki.

Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki, ametajwa waziri bora zaidi katika utendakazi , katika ripoti mpya iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya Politrack.

Mwenzake wa kilimo Mithika Linturi, aliibuka wa pili, huku kampuni hiyo ikiashiria mageuzi katika sekta ya kilimo, kama vile dijitali ambayo yamechochea ukuaji katika kilimo.

Kulingana na kampuni hiyo ya Politrack Africa, waziri wa  ushirika Simon Chelugui, aliorodheshwa wa tatu huku waziri wa biashara na uwekezaji Rebecca Miano akiibuka wa tano.

“Huku baadhi ya mawaziri wakioyesha uongozi mwema, uvumbuzi wa sera na utoaji huduma, baadhi ya mawaziri wamekumbwa na changamoto zikiwemo, utumizi mbaya wa fedha za umma na kutoafikia matarajio ya umma,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo leo Alhamisi.

Website | + posts