Home Burudani Portable matatani baada ya kuonekana kwenye video akidhulumu mhubiri

Portable matatani baada ya kuonekana kwenye video akidhulumu mhubiri

0
kra

Mwanamuziki wa Nigeria Portable ambaye jina lake halisi ni Habeeb Olalomi Badmus amezua ghadhabu kali kati ya watumizi wa mitandao nchini Nigeria.

Video hiyo inamwonyesha akimzaba kofi mhubiri wa barabarani ambaye alikuwa anahubiri nje ya eneo analomiliki la kuuza pombe kwa jina “Odogwu Bar” katika jimbo la Ogun.

kra

Tukio hilo ni la jana Jumatatu Septemba 9, 2024 na Portable ambaye alipata umaarufu kupitia kibao chake cha Zazu alikuwa katika eneo hilo akiwasiliana na wafuasi wake wa Instagram mubashara.

Aliposikia mhubiri huyo akihubiri alituma mmoja wa wasaidizi wake amkanye lakini mhubiri akaendelea kupaaza sauti.

Kulingana naye, mhubiri huyo hakumletea lolote la manufaa kwani katika biashara hiyo yake anachotaka ni pesa.

Aliongeza kwamba kabla ya kutoka nyumbani alijiombea na wakati huo ulikuwa wa kuuza pombe.

Yeye mwenyewe alilazimika kuenda kukabiliana na mhubiri huyo ndiposa akamzaba kofi.

Wafuasi wake wamemzomea sana mitandaoni wakisema kwamba ameingiwa na kiburi baada ya kupata hela nyingi kutokana na muziki wake.

Hii sio mara ya kwanza mwanamuziki huyo anahusika kwenye vurugu. Yapata mwezi mmoja uliopita alinakiliwa kwenye video akimpiga shabiki wake mmoja.

Portable alikuwa ameenda kuhudhuria hafla ya mazishi katika eneo moja nchini Nigeria ndiposa akajipata kwenye majibizano na shabiki huyo.

Alionekana kwenye hiyo video akimsukuma shabiki huyo akaanguka kwenye mtaro na kuumia naye akaingia kwenye gari lake na kuondoka.

Waliokuwepo walisikika wakimfokea Portable huku wengine wakimtukana.

Website | + posts