Home Habari Kuu Polisi wazindua sare mpya

Polisi wazindua sare mpya

0

Huduma ya Polisi imezindua sare mpya zenye majina na nambari za maafisa huku wale wa kike wakiwa na sketi na suruali ndefu.

Sare hizo mpya za rangi ya samawati iliyokoza zinabadilishwa na zile ambazo zimekuwepo tangu mwaka 2018.

Jopokazi la kutathmini mabadiliko katika kikosi cha polisi kilichoongozwa na Jaji mstaafu David Maraga, kwenye ripoti yake lilipendekeza kurejeshwa kwa sare za awali.

Hata hivyo polisi wa utawala,wale wa misitu na GSU watasalia na sare zao .

Sare hizo mpya zimetengezwa nchini kwa kutumia vitambaa vinavyoundwa nchini  kutoka maeneo ya Thika, Kitui, Nakuru na  Eldoret katika kampeini ya serikali ya kuhimiza matumizi ya vitu na mavazi yanayotengezwa nchini na kuinua viwanda vyetu.