Home Kimataifa Polisi wawakamata washukiwa wawili wa ugaidi Moyale

Polisi wawakamata washukiwa wawili wa ugaidi Moyale

Washukiwa hao walikiri kwamba walikuwa njiani kwenda Somalia kujiunga na kundi la Al-Shabaab, baada ya kusajiliwa katika nchi moja jirani.

0
Washukiwa wawili wa ugaidi wakamatwa na polisi.
kra

Maafisa wa upelelezi wamewakamata washukiwa wawili wa ujambazi. Kwenye taarifa,idara ya upelelezi DCI,imesema  Abdirahman Shaffi Mkwatili aliye na umri wa miaka 25 na Sadam Jafari Kitia aliye na miaka 30 walikamatwa Moyale wakiwa njiani kwenda Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Duru zinarifu kwamba washukiwa hao walikuwa na kijitabu kilichokuwa na maandishi ya lugha ya Kiswahili, ambacho walikuwa wakitumia kuwaelekeza kwenye safari yao kutoka Tanzania hadi mjini Jilib nchini Somalia.

kra

Washukiwa hao walikiri kwamba walikuwa njiani kwenda Somalia kujiunga na kundi la Al-Shabaab, baada ya kusajiliwa katika nchi moja jirani.

Kukamatwa kwa washukiwa kumejiri wiki mbili baada ya raia wengine watatu wa Tanzania, Abdul Saif Salimu, Zuberi Ngare Mtondoo na Seif Abdalla Jumawere kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi.

Raia mmoja wa Uganda pia alikamatwa hivi majuzi katika eneo la Liboi,akiwa njiani kwenda Somalia.

Wenye magari ya uchukuzi wa abiria pia wametakiwa kuwa waangalifu na kuwaripoti kwa polisi abiria wanaowashuku.