Home Habari Kuu Polisi waua wezi wanne wa mifugo Samburu

Polisi waua wezi wanne wa mifugo Samburu

0

Wezi wanne wa mifugo wameuawa katika kaunti ya Samburu na polisi kwenye shambulizi la kushtukiza baada ya wezi hao kumuua afisa mmoja wa polisi .

Wezi wengine wa mifugo walifanikiwa kutoroka huku polisi wakipata na kurejesha ng’ombe waliokuwa wameibwa kutoka kaunti ya Meru.

Polisi mmoja aliuawa siku kuu ya Krismasi wakati polisi walikuwa wakiwakimbiza wezi wa mifugo katika eneo la Achers kauntiu ya Samburu, baada ya kuzuka kwa makabiliano kati ya polisi na gene hilo.

Ngombe hao wapatao 100 walirejeshwa Ijumaa katika kitu cha Posta kaunti ya Laikipia katika hafla iliyoongozwa na naziri wa usalama taifa Kithure Kindiki.

Website | + posts