Polisi walinasa pombe haramu katika kaunti ya Kiambu siku ya Ijumaa na kuwatia mbaroni washukiwa kadhaa .
Kulingana na ripoti ya polisi washukiwa walikuwa wamepakia pombe hiyo haramu kwa nembo ya vileo vingine huku pia lita 240 za pombe aina ya Spirits zilizopakiwa kwa madumu zikipatikana.
Pombe hiyo ilikuwa na nembo bandia za KRA na ikiwa imepakiwa kwa zaidi ya chupa 1,000 za pombe tofauti .