Home Kimataifa Polisi wanasa bunduki haramu kaunti ya Marsabit

Polisi wanasa bunduki haramu kaunti ya Marsabit

0
Polisi wanasa Bunduki haramu kaunti ya Marsabit.
kra

Maafisa wa polisi kaunti ya Marsabit wamepata bunduki haramu na kumtia nguvuni mshukiwa wakati wa operesheni ya kiusalama iliyowalenga washukiwa wa mauaji katika kata ya Kargi, kaunti ndogo ya Loiyangalani.

Afisa mkuu wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinani kaunti ya Marsabit Luka Tumbo, aliripoti kuwa bunduki aina ya AK-47 ikiwa na risasi 10, ilipatikana katika eneo la Manyatta Ngolop.

kra

Washukiwa hao wanatafutwa kuhusiana na mauaji ya mwananmke mkongwe Februari 18, aliyedaiwa kuhusika na uchawi.

Licha ya kuwa washukiwa hao walifanikiwa kutoroka, mwanamume mwenye umri wa miaka 30 aliyepatikana na bunduki hiyo, alitiwa nguvuni na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central Marsabit mjini.

“Operesheni hiyo ilizaa matunda kwa kuwa tulipata bunduki haramu na risasi kumi,” alisema Tumbo.

Kaimu kamishna wa kaunti ya Marsabit David Saruni, alipongeza maafisa hao wa usalama, huku akiwataka kuongeza juhudi katika kukabiliana na uhalifu.

Alitoa wito kwa wakazi kushirikiana na maafisa wa utawala kwa kutoa habari zitakazosaidia kuwatia nguvuni washukiwa hao.

Website | + posts