Home Habari Kuu Polisi wakanusha madai ya kukamatwa kwa Gavana Mwangaza

Polisi wakanusha madai ya kukamatwa kwa Gavana Mwangaza

0

Huduma ya taifa ya polisi nchini NPS imekanusha madai kwamba Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza alikamatwa.

Kwenye taarifa kupitia akaunti iliyothibitishwa ya huduma ya taifa ya polisi kwenye mtandao wa X, polisi wamekanusha taarifa hizo bila kutoa maelezo zaidi.

Picha zilisambazwa mitandaoni zikionyesha Gavana Mwangaza akiwa ndani ya gari ya maafisa wa polisi na taarifa kwamba alikamatwa kwenye mkutano wa mpango wake wa kusaidia jamii wa Okolea.

Website | + posts