Home Kaunti Polisi wachunguza wizi wa vifaa katika bunge la kaunti ya Kisumu

Polisi wachunguza wizi wa vifaa katika bunge la kaunti ya Kisumu

0

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kubaini walioingia bila idhini katika majengo ya bunge la kaunti ya Kisumu na kuiba runinga na vifaa vya sauti vikiwemo vipaza sauti wikendi iliyopita.

Spika wa bunge hilo Elisha Oraro alithibitisha kisa hicho kupitia taarifa akisema kwamba uchunguzi unaendelea kwa nia ya kuwakamata wahusika na kupata mali iliyoibwa.

Oraro alisema watatumia njia zote katika uchunguzi ikiwa ni pamoja na picha za kamera fiche na vyanzo vingine vya habari kufahamu na kuwakamata wahusika wa kisa hicho. Ana uhakika kwamba watafanikiwa wakiwa na usaidizi wa maafisa wa usalama.

Aliongeza kuwa vikao vya bunge vitaendelea kama kawaida akisema kumbukumbu za mijadala ya bunge hilo, yaani Hansard, ambazo ni muhimu kwao hazikuharibiwa.

Kulingana naye, bunge la kaunti ya Kisumu halitashtuliwa na visa vya wahalifu wanaotaka kulemaza utoaji huduma kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Bunge hilo sasa limeamua kuratibu upya mipango ya ulinzi kufuatia kisa hicho.

Oraro anasihi Wakenya ambao huenda wanajua lolote kuhusu kisa hicho wajitokeze kusaidia maafisa wa polisi katika uchunguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here