Home Kaunti Polisi wachunguza kisa cha moto katika shule ya msingi ya Igoji

Polisi wachunguza kisa cha moto katika shule ya msingi ya Igoji

Kumekuwa na mzozo kuhusu umiliki wa ardhi hiyo ya ekari 33, kati ya kanisa katoliki na serikali ya kaunti ya Meru.

0
kra

Maafisa wa polisi kaunti ya Meru wanachunguza kisa cha moto kilitochotokea katika shule ya msingi ya Igoji.

Washukiwa wanane walifikishwa katika mahakama ya Nkubu jana Jumatatu, baada ya kutuhumiwa kuteketeza shule hiyo.

kra

Kulingana na Kamishna wa kaunti ya Meru Jacob Ouma aliyezuru shule hiyo akiwa ameandamana na maafisa wengine wa kaunti hiyo, alisema moto huo ulisababisha hasara ya mamilioni ya pesa, akidokeza kuwa hakuna visa vya majeruhi kwa kuwa wanafunzi wako likizo.

Kumekuwa na mzozo kuhusu umiliki wa ardhi hiyo ya ekari 33, kati ya kanisa katoliki na serikali ya kaunti ya Meru.

Hakimu Mkuu R. Ongira aliagiza washukiwa hao wazuiliwe rumande baada ya wao kukanusha mashtaka dhidi yao.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 15, 2024.

Website | + posts