Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei ameagiza maafisa wa polisi kukamata magari yote ambayo yana ving’ora na taa za kumwekamweka bila idhini.
Kulingana na Koskei magari yaliyoidhinishwa kutumia vifaa hivyo ni pamoja na yale ya maafisa wa polisi, ya kuzima moto, ambulensi na mengine.
Vifaa hivyo alisema vinatumiwa wakati wa dharura na ni vya kuhakikisha usalama wa umma.
wanaotaka kuweka ving’ora na taa za kumwekamweka kwenye magari yao wameshauriwa kutafuta idhini kwa kufuata taratibu zilizoko.
Koskei aliwashauri maafisa husika katika bunge, idara ya mahakama, serikali za kaunti na tume huru zilizobuniwa na katiba kutoa vifaa hivyo kwenye magari ya maafisa wao.