Home Kimataifa Polisi wa Trafiki wakamatwa kwa kuchukua hongo Kericho

Polisi wa Trafiki wakamatwa kwa kuchukua hongo Kericho

0
kra

Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC wamekamata maafisa wawili wa polisi wa trafiki katika kituo kimoja kinachofahamika sana cha kuchukua hongo katika kaunti ya Kericho.

Wawili hao Rachael Aiyabei na John Oluoch walikamatwa kwenye kituo hicho mjini Litein kwenye barabara kuu ya kutoka Sotik kuelekea Kericho.

kra

Ikithibitisha kukamatwa kwa maafisa hao, tume ya EACC kupitia kwa msemaji wake Eric Ngumbi, ilielezea kwamba hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia lalama za kila mara za polisi wa trafiki kuchukua hongo kutoka kwa waendeshaji magari na wakenya wengine kwa kisingizio cha kutekeleza sheria za trafiki.

Washukiwa hao walikamatwa Jumanne jioni, wakashughulikiwa katika afisi za EACC tawi la South Rift jijini Nakuru Jumatano. Waliachiliwa kwa dhamana wakisubiri uchunguzi ukamilike.

EACC inakumbusha umma kwamba hata ingawa wengi wao huchukulia hongo kuwa ufisadi wa kiwango cha chini, madhara yake ni makubwa kwa sababu inaingilia usalama wa barabarani na kuhatarisha maisha.

Kutofuata sheria za trafiki kwa sababu mtu ametoa hongo ni kisababishi kikuu cha ajali za barabarani zinazoshuhudiwa kwenye barabara kuu nchini hasa zinazotoka Nairobi kuelekea magharibi mwa nchi.

Website | + posts