Home Kimataifa Polisi wa Kenya wapiga hatua kubwa nchini Haiti

Polisi wa Kenya wapiga hatua kubwa nchini Haiti

0
kra

Polisi wa Kenya wamepiga hatua kubwa miezi miwili tangu waanze misheni ya kushika doria na kurejesha hali ya utulivu mjini Port-au-Prince nchini Haiti.

Kundi hilo la maafisa wa polisi kutoka makundi mbalimbali, maarufu kama MSS, wakishirikiana na polisi wa kitaifa nchini Haiti, wamefanikiwa kurejesha utulivu na kutwaa miundimbinu muhimu ikiwemo uwanja wa ndege uliokuwa mikononi mwa magenge, kufungua barabara zilizofungwa na kuwarejesha makwao raia waliofurushwa.

kra

Kulingana na taarifa ya kaimu Inspekta Mkuu wa Polisi Robert Masengeli, huduma ya taifa ya polisi, NPS, itaendelea kuwaunga mkono polisi wa kenya nchini Haiti.

Polisi hao walio nchini Haiti wataendelea kupokea mishahara yao kutoka NPS huku malipo ya marupurupu yao yakikaribia kukamilika.

Masengeli amempongeza kamanda wa ujumbe wa kenya nchini Haiti Godfrey Otunge kwa ufanisi huo akiahidi kuendelea kushirikiana naye kwa karibu.

Website | + posts