Home Habari Kuu Polisi wa Kenya waahidi kuendelea kusaidia wenzao wa Haiti kudumisha amani

Polisi wa Kenya waahidi kuendelea kusaidia wenzao wa Haiti kudumisha amani

0
kra

Kikosi cha maafisa wa polisi wa Kenya kilichoko Haiti kimesisitiza kujitolea kwake kuendelea kushirikiana kwa karibu na polisi wa Haiti kutekeleza jukumu lao la kurejesha utulivu katika nchi hiyo.

Haya yalidhihirika kwenye taarifa fupi iliyochapishwa kwenye akaunti ya X ya huduma ya taifa ya polisi.

kra

Inaarifiwa pia kwamba balozi wa Marekani nchini Haiti Linda Thomas-Greenfield, alizuru kikosi cha mataifa mbali mbali kinachoongozwa na Kenya nchini Haiti mnamo Julai 19, 2024.

Kufikia sasa kikosi hicho kikosi hicho kinaripotiwa kuafikia ufanisi hatua kwa hatua kwa lengo la kuhakikisha kwamba Haiti inakombolewa kutokana na utawala wa magenge yaliyojihami.

Kikosi hicho kimefanikiwa kurejesha usimamizi wa bandari ya APN kwa serikali ya Haito huku kikiondoa vizuizi vya barabarani vilivyokuwa vimewekwa na magenge kwenye barabara ya kuelekea Ganthier.

Mkuu wa baraza la mpito nchini Haiti Edgard Leblanc, naye alizuru kikosi hicho Ijumaa Julai 26, 2024 kutokana na hatua ambazo kimepiga tangu kilipowasili nchini Haiti.

Kenya imetuma maafisa wa polisi zaidi ya 600 nchini Haiti kama sehemu ya mpango wa kutuliza vurugu zinazosababishwa na magenge yaliyojihami nchini humo.

Magenge hayo yamesababisha watu zaidi ya laki 5 kupoteza makazi huku watu karibu milioni tano wakikumbwa na njaa.

Kenya inaongoza kikosi hicho cha mataifa mbali mbali cha kusaidia kurejesha usalama na utulivu nchini Haiti huku wanachama wengine wakiwa wa nchi kama Benin, Barbados, Chad na Bangladesh.

Website | + posts