Home Kaunti Polisi Nairobi wapata simu 354 zilizoibwa

Polisi Nairobi wapata simu 354 zilizoibwa

Maafisa hao kutoka kituo cha polisi cha Kayole, Jumamosi asubuhi walinasa simu 354, zilizokuwa zikisafirishwa kwa gari aina ya Toyota Premio, mtaani Umoja.

0
Polisi wanasa simu zilizoibwa Jijini Nairobi.

Mwanamume mmoja amekamatwa jijini Nairobi baada ya maafisa wa polisi kunasa simu za rununu zinazoshukiwa kuwa ziliibwa.

Maafisa hao kutoka kituo cha polisi cha Kayole, Jumamosi asubuhi walinasa simu 354 zilizokuwa zikisafirishwa kwa gari aina ya Toyota Premio mtaani Umoja.

Mshukiwa kwa jina Dennis Kioko Mutua kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kayole akisubiri kufikishwa mahakamani.

“Mnamo tarehe 25/11/2023 maafisa wa huduma ya taifa ya polisi kutoka kituo cha polisi cha Kayole, walipata simu za rununu 354 katika gari lenye nambari za usajili KAZ 505F aina ya Toyota Premio mtaani Umoja, na kumkamata mshukiwa mmoja DENNIS KIOKO MUTUA ambaye anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kayole akisubiri kufikishwa mahakamani,” ilisema taarifa ya polisi kupitia mtandao wa X.

Website | + posts