Home Kimataifa Polisi Meru washiriki mazungumzo na wanabodaboda

Polisi Meru washiriki mazungumzo na wanabodaboda

0
kra

Maafisa wa polisi wa kaunti ndogo ya Igembe kaskazini katika kaunti ya Meru wameanzisha mpango wa kushirikisha waendeshaji pikipiki za uchukuzi almaarufu bodaboda, kwa lengo la kukabiliana na visa vya uhalifu katika eneo hilo.

Wanabodaboda wa eneo la Laare walifanya mkutano na maafisa wa polisi kutoka vituo vya Mutuati na Laare, Naibu OCPD wa Laare na mbunge wa eneo hilo ambapo walijadiliana kuhusu namna ya kushirikiana kutokomeza uhalifu.

kra

Maafisa wa polisi waliwataka waendeshaji pikipiki hao wawe wakitoa taarifa kwao kuhusu wahalifu ili wachukue hatua za haraka kuwazuia wasitekeleze visa vya uhalifu.

Waliombwa wajiepushe na uhalifu hasa baada ya baadhi yao kuhusishwa na visa vya uhalifu awali.

Mbunge wa eneo hilo Julius Taitumu kwa upande wake aliwataka wahudumu hao wa uchukuzi wa umma washirikiane na maafisa wa ulinzi katika eneo hilo.

Maafisa hao wa polisi waliamua kuchukua hatua hiyo kufuatia kuongezeka kwa visa vya uhalifu nivavyohusishwa na wana bodaboda pamoja na wizi wa pikipiki.

Ripoti yake Jeff Mwangi

Website | + posts