Home Habari Kuu Polisi afariki katika ajali ya barabarani

Polisi afariki katika ajali ya barabarani

0

Afisa wa trafiki katika kaunti ya Bungoma ameripotiwa kufariki baada ya kugongwa na gari la polisi, lililokuwa likiendeshwa kwa kasi katika makutano ya barabara ya Cheptais.

Ripoti ya polisi imeeleza kuwa, Fredrick Juma wa kituo cha Bungoma Magharibi, alikumbana na mauti yake akiwa kazini siku ya jumapili alipokuwa akikagua trela na ghafla akagongwa na gari la polisi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.

Imefahamika kuwa, dereva Gideon Magut wa gari la polisi la Sirisia alishindwa kulidhibiti na kumgonga Fredrick akijaribu kukwepa kugongana na gari la mizigo lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Life Care ukisubiri kufanyiwa upasuaji .

Kwingineko,Polisi wanachunguza kisa cha askari Paul Macharia wa kituo cha Ololulunga katika kaunti ya Narok ambaye alijeruhiwa na kupoteza fahamu.

Polisi walihoji kuwa, mwathiriwa alishambuliwa usiku wa tarehe nane na tisa na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake iliyoko karibu na soko la Olulunga, na alipatikana na majeraha ya kukatwa kichwani huku akivuja damu.

Boniface Musotsi
+ posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here