Home Habari Kuu Polisi 42,000 kuhamishwa kuanzia wiki ijayo, asema Kindiki

Polisi 42,000 kuhamishwa kuanzia wiki ijayo, asema Kindiki

0

Maafisa wa polisi zaidi ya 42,000 ambao wamehudumu katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatarajiwa kuhamishwa ifikiapo Jumatano wiki ijayo. 

Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki.

Kindiki amesema uhamishaji wa polisi hao 42,500 unatarajiwa kuongeza utendakazi wao akitaja kuzembea kwa wengi wao kazini kuwa sababu ya hatua hiyo.

Waziri amesema kuwa maafisa wa polisi waliohudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kituo kimoja hawana uwezo wa kutekeleza sheria mpya za msako dhidi ya pombe haramu.

Hatua hiyo inatarajia kuigharimu serikali kwani italazimika kuwalipa maafisa hao marupurupu ya usumbufu kabla ya kuwahamisha.

Haya yanajiri kufuatia sheria kali zilizowekwa na serikali ya kitaifa kukabiliana na wanaogema na kuuza pombe haramu.

Website | + posts