Klabu ya Police FC imekamilisha mazoezi yake jumamosi jioni uwanjani Nyayokujiandaa kwa mechi ya mchujo mkumbo wa kwanza, kuwania kombe la shirikisho Afrika dhidi ya klabu ya Coffee kutoka Ethiopia.
Pambano hilo litasaktwa Jumapili alasiri katika uchanjaa wa kitaifa wa Nyayo.
Maafande hao wanashiriki kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza ya baada, ya kunyakua kombe Mozzart msimu uliopita.
Marudio yataandaliwa juma lijalo huku mshindi wa jumla, akijikatia tiketi kwa raundi ya kwanza.